Sunday, February 9, 2014

KILICHOJIRI MKUTANO WA MWAKA 2013 WA WANACHAMA WA SACCOS UCC

Mkutano  mkuu   wa  mwaka  wa  chama  cha  kuweka  na  kukopa  cha  wafanyakazi  wa   UCC  ulifanyika   jumamosi  tarehe  08  February  2014, pamoja  na    agenda   zingine , ilikuwepo  agenda uchaguzi  wa wajumbe  wa  bodi  na  kamati  ya usimamizi.  

 
Mwenyekiti  wa  UCC  Saccos   Mr Prudence Ongera (aliyesimama)  akifungua  mkutano  wa   wanachama  wa  chama  cha  hiari 
cha  kuweka  na  kukopa  cha  wafanyakazi  wa  UCC, wengine  ni   Mkurugenzi Mtendaji wa UCC  Dr  Ulingeta   O.  Mbamba(aliyekaa kushoto)  
ambaye ni Mlezi  wa  chama na Ms.  Geritha   Magusi  ambaye ni Karani wa
Mahesabu wa UCC SACCOS.
.
 Sehemu  ya   wanachama   waliohudhuria    mkutano  .
Mr  Ahmed  Bori    mwanachama  toka  tawi  la  Dodoma  akisalimiana  na  mwenyekiti, chama  kitaandaa  utaratibu  wa  kuleta 
wawakilishi    toka  matawi   nje  ya  Dar wakati  wa  mkutano  mkuu  wa  mwaka 2014.

 Mr   Michael  S   Abdallah   akishawishi  wanachama  wampigie  kura  kwa  nafasi  ya  ujumbe  katika  kamati  ya  usimamizi    wa  chama,  aliibuka    kidedea    kwa  kura  28   za  ndiyo   kati  ya  31.

KWA  PICHA  NA  MATUKIO  MENGINE  WAKATI  WA  KIKAO     TEMBELEA
           >>>>>

Friday, February 7, 2014

Hafla ya Kuwakaribisha Wanafunzi wapya muhula mpya Feb - June 2014 Yafanyika Mbezi Branch.


UCC  leo  imezindua  rasmi  kuanza  kwa    masomo   ya  muhula  wa  kwanza  wa  masomo  Feb -  June  2014   katika  hafla (Orientation)  iliyofanyika  katika  ukumbi    wa    maktaba   tawi  la  Mbezi  Beach, zaidi  ya  wanafunzi  wapya  wapatao 300  wamehudhuria
 Principal Training  Services/ Manager  Operations  Dr  Geofrey  Karokola  akiwakaribisha   sehemu  ya  wanafunzi  wapya , pembeni  ni  meneja wa  tawi la  Mbezi  Mr Antony  Karokola.
Picha  ya  pamoja  baadhi  ya  wafanyakazi  wa  UCC    na  wanafunzi    wapya .

 Mr Antony Karokola  akitoa  utambulisho   kwa  wanafunzi.
Sehemu  ya  wanafunzi  wapya  kwa   umakini  wakifuatilia  maelekezo.

Picha   zaidi ......